24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Sanchez aipeleka Chile robo fainali

RIO, BRAZIL

BILA kujali kusumbuliwa na enka, mshambuliaji wa timu ya taifa Chile, Aleix Sanchez, amefanikiwa kuipeleka timu hiyo robo fainali ya michuano ya Copa America inayoendelea nchini Brazil.

Usiku wa kuamkia jana Chile walishuka dimbani katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya Ecuador na kufanikiwa kushinda mabao 2-1.

Sanchez alikuwa anacheza mchezo huo huku akiwa na maumivu ya enka baada ya kuumia katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, ambapo timu hizo zilikwenda mapumziko huku zikiwa zimefungana bao 1-1.

Baada ya kipindi cha pili kuanza, bado mchezaji huyo alikuwa na maumivu lakini alipambana na kufanikiwa kuifungia bao la pili katika dakika ya 51 lililowafanya waweze kufuzu na kuingia hatua ya robo fainali.

Mchezo wa kwanza Chile ilifanikiwa kushinda mabao 4-0 dhidi ya Japan, huku Sanchez akifunga bao la mwisho. Chile ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo ikiwa wamechukua taji hilo mara mbili mfululizo.

“Nilikuwa nacheza huku nina maumivu ya enka, lakini ilinibidi nijikaze kwa ajili ya kuipenda nchi yangu, siku zote nikiwa nacheza mpira na jezi ya timu ya taifa ninacheza nikiwa na furaha kubwa sana,” alisema mchezaji huyo.

Sanchez mbali na kuwa kwenye kiwango kizuri akiwa na uzi wa Chile, lakini mchezaji huyo amekuwa na kipindi kigumu ndani ya klabu yake ya Manchester United, huku akidaiwa kucheza chini ya kiwango tangu alipojiunga mwaka 2018.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, anaongoza kwa kulipwa kiasi kikubwa cha mshahara ndani ya Manchester United, lakini amekuwa akikosa namba ya kudumu mara kwa mara, lakini anaamini kwenye michuano hiyo ya Copa America itamfanya kurudisha kiwango chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi.


- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles