23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Misri waipigia ‘saluti’ Zimbabwe

Wachezaji wa timu ya taifa Misri, wakishangilia bao juzi katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Zimbabwe. Mchezo huo ulimalizika kwa Misri kushinda bao 1-0.

CAIRO, MISRI

BAADA ya timu ya taifa ya Misri kufanikiwa kuanza na ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON), kocha wa timu hiyo Javier Aguirre, ameipigia saluti Zimbabwe kutokana na kiwango walicho kionesha.

Pazia la michuano hiyo lilifunguliwa juzi kwa mchezo mmoja kupigwa, ambapo Misri walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe, bao la pekee lilifungwa na Mahmoud Trezeguet, lakini wapinzani hao walionesha kiwango cha hali ya juu na kuwashangaza wengi.

Misri walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mabao zaidi ya mawili kupitia kwa nyota wao Mohamed Salah, Marwan Mohsen na Abdallah El-Said, lakini mlinda mlango wa Zimbabwe, Edmore Sibanda.

Aguirre, ameweka wazi kuwa, hana wasiwasi na kikosi chake, anaamini walishindwa kuwa kwenye ubora wao kwa kuwa ni mchezo wa kwanza, lakini michezo itayofuata watarudi kwenye ubora.

“Nimeridhishwa na kiwango walichokionesha wachezaj wangu, lakini tulipoteza nafasi nyingi sana hasa katika safu ya kiungo, wapinzani wetu walikuwa na kasi sana na kutusababishia matatizo, lakini kiwango chao kilikuwa bora zaidi katika kipindi cha pili, hivyo naweza kusema walikuwa wamejipanga vizuri.

“Bao letu liliwafanya Zimbabwe kuwa kwenye kiwango kizuri kwa kuwa hakuwa na kitu cha kupoteza, hivyo muda wote walikuwa wanatushambulia, tunatarajia kuyafanyia kazi mapungufu yetu,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles