22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

HAKIMU: KESI YA LWAKATARE NI MAAJABU

Na Kulwa Mzee -Dar es Salaam


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imesema kinachoendelea katika kesi ya kula njama ya kudhuru kwa sumu, inayomkabili Mkurugenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake, ni maajabu matupu.
 Hayo yalibainika jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa huku Inspekta wa Polisi, Hamisi Saidi akidai upelelezi haujakamilika.


Baada ya Inspekta Saidi kudai upelelezi haujakamilika, Hakimu Simba alitaka kupata maendeleo ya kesi hiyo. Haikufahamika upelelezi umefikia wapi.


“Kinachoendelea hapa maajabu matupu, kesi ilifikishwa mara ya kwanza Machi 20 mwaka 2013, imetajwa mahakamani mara nyingi.
“Machi 20 mwaka 2013 mpaka leo kesi ilishaahirishwa mara ngapi, kama wanafungwa wafungwe na kama wanaachiwa waachiwe, kesi zinakuwa haziendelei… haipendezi, ikija mara nyingine kama bado nitawarudishia watuhumiwa wenu muondoke nao,” alisema Hakimu Simba.

Hakimu Simba alipokea taarifa kutoka kwa mdhamini wa Lwakatare, kwamba ni mgonjwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, hivyo aliagiza apewe taarifa ya tarehe nyingine ya kesi.
Kesi iliahirishwa hadi Aprili 14, mwaka huu kwa kutajwa.    


Lwakatare na Ludovick Joseph wanadaiwa Desemba 28, mwaka 2013 katika eneo la King’ong’o, Wilaya ya Kinondoni kwa pamoja walikula njama za kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles