MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Antoine Griezmann, alilazimika kukata sehemu ya mshahara wake ili arudi Atletico Madrid.
Kwa mujibu wa taarifa, Griezmann amepunguza asilimia 40 ya mshahara aliokuwa akilipwa na Barcelona.
Griezmann alijizolea umaarufu mkubwa wa upachikaji mabao akiwa Atletico lakini alijikuta kwenye wakati mgumu alipohamia Barca mwaka juzi.
Kilichomfanya ashindwe kuwika Camp Nou na kufunga mabao 35 pekee katika mechi 102 ni mfumo uliomlazimisha kutocheza mshambuliaji wa kati ili kumpisha Lionel Messi aliyekuwa hatari kwenye eneo hilo.