23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

GRACA MACHEL AKEMEA NDOA ZA UTOTONI

Na TIMOTHY ITEMBE- BUTIAMA 


MJANE wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, marehemu Nelson Mandela, Graca Machel, amekemea ndoa za utotoni  na ukeketaji kwa watoto wa kike, unaoendelezwa na baadhi ya mila za makabila nchini.

Graca amesema vitendo hivyo kwa karne ya sasa havina nafasi.

Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani hapa alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyamisisi.

Alisema suala la ukeketaji halitakiwi kupewa nafasi kwani linaminya haki za mtoto wa kike.

Mjane huyo wa Mandela yuko mkoani Mara kwa ziara ya siku tatu, kutembelea mradi wa watoto walio nje ya mfumo wa shule unaotekelezwa na Mara Alliance na Graca Machel Trust Fund.

Alisema lengo la ziara yake ni kujionea watoto walioibuliwa na mradi huo, hususan walioko chini ya umri wa miaka saba hadi 17, kuzungumza nao na kuangalia changamoto zinazowakabili.

 “Katika karne hii, kuna haja ya jamii yenye fikra mgando kubadilika na kuondokana na dhana potofu iliyojengeka katika vichwa vyao, kuwa mtoto wa kike hana thamani badala yake anatakiwa akeketwe ili aolewe,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anna   Nyamubi, alisema kuna mahitaji ya vyumba 1,762 vya madarasa, huku idadi ya wanafunzi ikiwa 6,480.

Alisema changamoto zinazowakumba wanafunzi ni utoro ambao unatokana na wazazi na mimba za utotoni.

Nyamubi alisema jamii mkoani Mara inaendekeza mila kuliko masomo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya watoto na kuwakwamisha katika taaluma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles