26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Gharama za usafiri, kikwazo watanzania kutembelea hifadhi

Na Derick Milton, Serengeti

Licha ya serikali kupunguza kwa kiwango kikubwa gharama kwa Watanzania kutembelea hifadhi za taifa, bado mwitikio imeendelea kuwa mdogo wa kutembelea hifadhi hizo kutokana na uwepo wa gharama kubwa zinazotozwa za usafiri ndani ya hifadhi.

Moja ya hifadhi ambayo Watanzania wamekuwa na mwitikio mdogo kuitembelea ni hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambapo kikwazo kikubwa ni uwepo wa gharama kubwa zinazotozwa kwa ajili ya kupata usafiri wa kutembelea wakiwa ndani ya hifadhi hiyo.

Akiongea na Waandishi wa Habari wa mkoa wa Simiyu waliotembelea hifadhi hiyo Jana, James Nahonyo Afisa uwifadhi Idara ya utalii hifadhi ya Taifa ya Serengeti alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiogopa gharama za usafiri wanazotakiwa kutoa kwa ajili ya kutembelea hifadhi hiyo.

Nahonyo alisema kuwa serikali imepunguza kwa kiwango kikubwa tozo ya kuingia kwa Mtanzania, lakini pia akieleza kuwepo kwa huduma za malazi na chakula zenye gharama nafuu kwa Mtanzania ndani ya hifadhi hiyo.

” Bado tatizo lipo kwenye gharama za usafiri ambazo ndizo wengi wamekuwa wakielezea kuwa kikwazo kikubwa kwao kushindwa kutembelea hifadhi yetu, tumekuwa tukitoa Elimu ya mara kwa mara kuwahimiza watanzania kutembelea hifadhi yao, lakini wengi wanasema wanaogopa gharama za usafiri,” alisema Nahonyo……

“Tumekuwa tukiwaelimisha kuwa ili waweze kupambana na changamoto hiyo, wanaweza kuungana na kukodi magari kwenye maeneo yao ili kupunguza gharama, na tumeendelea kuwaelimisha kupenda raslimali za nchi yao,” alieleza Nahonyo.

Aidha Ofisa huyo alisema kuwa hifadhi hiyo ya Serengeti imeanzisha mkakati wa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao wanakoishi kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kutembelea hifadhi zao.

” Kama Serengeti katika kuhakikisha tunakuza utalii wa ndani, tumeanzisha mpango unaoitwa nyumba kwa nyumba, tumeanza na maeneo ambayo yanapakana na hifadhi hii, kuwataka wananchi waje lakini hata tasisi mbalimbali za umma na binafsi zitembelee hifadhi,” Alisema.

Ziara hiyo ya waandishi wa habari mkoa wa Simiyu iliyoratibiwa na Chama cha waandishi wa habari Mkoani humo (SMPC) ilijumuisha wanahabari 20 huku ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko ndani ya hifadhi hiyo.

Samila Yusuph mwandishi wa habari Kampuni ya Mwananchi Communication, alisema kuwa kupitia ziara hiyo wamepata uelewa mpana wa ikologia ya hifadhi hiyo pamoja na historia yake ikiwemo na vivutio mbalimbal

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles