27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Arusha yajipanga kuwekeza katika sekta ya utalii

Janeth Mushi,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha imekutana na wadau wa utalii kwa lengo la kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya utalii.

Akizungumza juzi katika kikao cha siku moja cha wadau, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk.John Pima amesema lengo la kikao hicho ni kujadiliana na kukaribisha fursa za uwekezaji hasa kutoka sekta binafsi ili kukuza utalii.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima.

Dk.Pima amesema kuna mambo mengi ambayo wadau wakishirikiana na serikali wataweza kuboresha mazingira na kuangalia namna wanaweza kurejesha hadhi ya Jiji la Arusha.

“Tunajaribu kuangalia namna ya kurudisha hadhi ya Arusha,tunakaribisha wadau kwani sisi tuna wataalam na nyie mna wataalam ila mna uzoefu zaidi hivyo tutaangalia kwa pamoja namna ya kuboresha na tutaweka mazingira mazuri ya kuwawezesha wawekezaji mkataokuwa tayari.

“Yapo mambo mengi ambayo tunamini sisi kama Jiji tukiyafanya kwa pamoja tutafanya vizuri zaidi,tunatka kutumia fursa hiyo kuboresha mazingira ya Arusha,tunataka tuone wageni wetu wanapofika Arusha wanakuwa na siku chache za kukaa Arusha na kufanya utalii wa kawaaida,wakae kwenye hoteli zetu na kufanua shughuli za kawaida,”amesema Dk.Pima.

Naye Meya wa Jiji la Arusha,Maximillian Iranghe amesema kwa sasa wamefungua milango kwa wawekezaji wote ambao wako ndani na nje ya Arusha na fursa zote zilizopo.

Meya wa Jiji la Arusha,Maximillian Iranghe

Amesema kuwa jiji hilo limeshindwa kuendelea katika baadhi ya mambo kutokana na urasimu uliokuwepo hivyo kwa sasa wamefungua milango kwa wawekezaji ili washirikiane namna ya kufanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya vivutio ikiwemo bonde la Mto Themi, Mto Naura, Mlima Suye pamoja na eneo maarufu la nyama choma ya mbuzi “Kwa Morombo”.

“Ukiona wakati mwingine Jiji la Arusha haliendelei ni kwa sababu ya urasimu ambao upo mahali hapa tuko hapa ili kuwaambia tumefungua milango mje kushirikina na tunajua huko nyuma kulikuwa na urasimu wa ajabu sana,Mwenyekiti ananiambia waliomba eneo la kujenga ofisi na kupewa taratibu zote akaambiwa mchakato unaendelea ila hadi sasa hawajajibwa ni miaka mine imepita.

“Arusha ulikuwa mji wa mchakato kila kitu mchakato,muda wa michakato umeisha sasa hivi ni muda wa kazi kwa matendo,tukiwa na vijana tukawa train kuuza jiji la Arusha tunaweza kufanya utalii kuwa mzuri na lengo langu mimi ni hizi hoteli ambazo zimelala zimekufa ziamke,watu wanadaiwa mikopo benki,kumbi za mikutano zinakufa,” amesema Iranghe.

Awali, Mwenyekiti wa Wakala wa Utalii nchini (TATO), Willy Chambulo,anataja baadhi ya masuala yaliyochangia kuharibu utalii katika jiji hilo ni pamoja na usafi wa mazingira pamoja na hali ya siasa.

“Kilichoharibu utalii Arush ni nini?Watalii walikuwa wanazagaa kila mahali,ili kuboresha huli lazima tuanze sisi wenyewe kwa kuhakikisha usafi wa mazingira.Matatizo mengine ya kisiasa unaharibu utaliu,kitu cha kwanza mtalii anataka kuhakikishiwa usalama wake.

“Sisi kama wafanyabiashara tunahitaji uwazi,wawekezaji wapo na fursa tumeshaziona.Msijiingize kwenye biashara nyie ainisheni maeneo hasa ya wazi na msiyauze,wapeni wafanyabiashara kwa masharti wayawekeze na hii itasaidia kukuza utalii,”amesema.

Wadau mbalimbali

Wakichangia mjadala huo baadhi ya wadau walioshiriki wa kikao hicho waliomba halmashauri hiyo kusimamia masuala mbalimbali ikiwemo ya usafi wa mazingira,pamoja na kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo.

Mmoja wa wadau hao Francisca Masika ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TATO,amesema umefika wakati wa halmashauri hiyo kutengeneza masoko ikiwemo meneo ya pembezoni ili kupunguza wafanyabiashara waliojaa pembezoni mwa barabara.

“Kwanini kama halmashuri  msianze kutengeneza masoko mbalimbali,ili wanaokaa barabarani waondoke ili watalii wanapokuja jiji lipitike,ukweli ni kwamba kwa sasa jiji halipitiki hata kama mnawapenda wanaanchi na mnataka kuwardhisha kwa sababu za kisiasa lakini hii imepitiliza,”

Kuhusu utalii,amesema kuwa siyo lazima kuanza na vitu vipya na badala yake wanaweza kuboresha vilivyopo ikiwemo kuboresha miundombinu. 

“Hizi barabara zilizojengwa zimetumia bilioni ngapi,mgeni akiniambia anataka kununua kitenge mjini nanza kujiuliza nitapaki gari wapi,nitatembea wapi,barabara zote zimekuwa masoko,”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles