25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri asisitiza TFF kuwekeza nguvu katika maeneo ya vituo vya michezo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amefanya Ziara katika Mradi wa Kujenga Kituo cha Michezo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF ulioko Kigamboni Kibada Jijini Dar es Salaam.

Waziri Bashungwa amefanya ziara hiyo leo akiwa ameongozana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu, Wallec Karia amekagua Mradi huo unaofadhiliwa na Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) Nnhini Tanzania ambao Umefanyika Kigamboni Dar es Salaam na Jijini Tanga, Waziri ameshuhudia shuguli za ujenzi zinavyoendelea na kujiridhisha na kutoa hari kwa Uongozi kufanikisha zoezi kwa kasi kwalengo la kumaliza kujenga viwanja vinne mapema mwisho wa Mwaka Huu.

Waziri ameisitizia TFF kwa awamu inayokuja ya fungu kutoka FIFA kuwekeza katika Maeneo mengine Nchini kwa kiwango kile kile kama Mradi wa Kigamboni na Tanga kwa kuzingatia hali ya kijiografia ya nchi yetu ili kutonyima fursa ya kujiendeleza kimichezo kwa Wananchi waishio mbali na Dar es Salaam na Tanga.

Kwa upande wa TFF Rais Karia aliorodhesha baadhi ya Huduma za kimicheo zitakazo kuwa zinapatikana hapo ambayo ni Mpira wa Miguu kwa viwanja vya Nyasi Bandia na Nyasi za Kawaida, Hoteli ya Hadhi ya Nyota Tatu, Hostel kwa Wakufunzi w Michezo na Wanamichezo, Viwanja vya mpira wa Wavu na Pete pia Kutakuwa na Mabwawa ya Kuogelea kwaajili ya Kuwanoa Wanamichezo wa Kuogelea nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles