Felis Mubibya atoa siri ya ‘He Is Real’

0
184

CHICAGO, MAREKANI

KUTOKA Chicago nchini Marekani, mwanamuziki mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felis Mubibya, amefurahishwa na ushirikano wake na mwimbaji wa Tanzania, Bella Kombo kwenye kolabo yao, He Is Real.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mubibya alisema licha ya umbali mkubwa uliopo kati ya Marekani na Tanzania ila anamshukuru Mungu wimbo wao, He Is Real uliweza kukamilika audio na video na sasa unapatikana mtandao.

 “He Is Real ni wimbo wa kumsifu Mungu ukimaanisha Mungu wetu ni halisi, ushirikiano huu wa Marekani na Tanzania ni mzuri hasa ukizingatia umebeba ujumbe wa kutia moyo, video tayari ipo katika chaneli yangu ya YouTube,” alisema Mubibya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here