‘Uweponi Mwako’ yawapaisha Jolly Twins

0
195

CHRISTOPHER MSEKENA

KUNDI la Jolly Twins limewashukuru wapenzi wa muziki wa Gospo kwa mapokezi mazuri ya wimbo wao, Uweponi Mwako ikiwa ni kazi yao ya pili baada ya Baba Eeh, waliomshirikisha Goodluck Gozbert.

Jolly Twins ni kundi linaloundwa na mapacha wawili wanaofanana, Martha na Maria wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo sasa wanaishi Queensland nchini Australia.

Martha ameliambia MTANZANIA kuwa anashukuru mapokezi ya kundi lao japo kuwa bado wanahitaji sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao wanaoishi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

 “Huu ni wimbo wa kumsifu Mungu, naamini mtu yeyote ambaye atausikiliza atabarikiwa, video tayari imetoka ipo kwenye chaneli yetu ya YouTube (Jolly Twins) pia imeanza kuchezwa kwenye redio na Tv mbalimbali kwahiyo kila mtu kwa nafasi yake akaitazame kwani hatabaki kama alivyo,” alisema Martha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here