26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

EU: SERIKALI YA UTURUKI ILIIBA KURA MILIONI 2.5

ISTANBUL, UTURUKI


WAANGALIZI kutoka Umoja wa Ulaya (EU), wanadai Serikali ya Uturuki ilichakachua kura milioni 2.5 zilizoiwezesha kushinda kura ya maoni kuhusu Katiba.

Matokeo ya mwisho yalimpa Rais Recep Tayyip Erdogan ushindi wa asilimia 51.41 na hivyo kuongeza mamlaka yake ya kirais.

Kwa mujibu wa mjumbe wa Austria aliyekuwa sehemu ya waangalizi hao, Alev Korun, kura milioni 2.5 ambazo hazikuwa katika bahasha zilijumuishwa katika mahesabu kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa sheria ya Uturuki, kura zilizo katika bahasha rasmi za uchaguzi ndizo zinazopaswa kuhesabiwa pekee.

Licha ya sheria hiyo, Korun aliwaambia wanahabari kuwa ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali alilazimisha kinyume na sheria kuhesabiwa pia kwa kura ambazo hazikuwa katika bahasha hizo.

Mjumbe huyo alisema uwezekano wa kuchezewa kwa kura kiasi hicho ni suala lenye uzito mkubwa, ambalo linaweza kubaditilisha matokeo.

Awali chama kikuu cha upinzani cha Republican People (CHP) pamoja na chama cha Wakurdi cha HDP, vimesema vitayapinga matokeo kutoka baadhi ya vituo, vikidai kulikuwapo udanganyifu.

Rais Erdogan ametupilia mbali ukosoaji huo.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake jana, Rais Erdogan aliwashambulia vikali waangalizi wa Ulaya.

“Kuna hawa waangalizi wa EU, walioandaa ripoti yao wenyewe eti uchaguzi wa Uturuki ulienda hivi na vile. Kwanza nawambia, jueni nafasi yenu. Hatuoni, hatusikii, wala hatuitambui ripoti yenu, tutaendelea katika njia yetu.

“Nyamazeni! Nchi hii imekwishafanya chaguzi nyingi za kidemokrasia ambazo hazijaonekana katika nchi yoyote ya Magharibi,” aliwakoromea.

Lakini licha ya malalamiko hayo, Rais Donald Trump wa Marekani alimpongeza Rais Erdogan kwa ushindi wake huo.

Aidha Trump alimsifu Erdogan kwa kuipongeza Marekani kwa kitendo chake cha kuitwanga mabomu Syria.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,926FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles