25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

FAMILIA 100 ZAMSHTAKI MKE WA MUGABE

HARARE, ZIMBABWE


FAMILIA zaidi ya 100 zilizotimuliwa na mke wa Rais Robert Mugabe, Grace kutoka makazi yao mashambani, zimeitaka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC kuingilia kati.

Hilo linakuja huku ripoti zikisema mahakama ilitoa hukumu kuzuia uamuzi huo wa Grace, ambaye anatafuta namna ya kupanua himaya yake ya kilimo katika eneo la Mazowe.

Baada ya wanakijiji wa Mazowe kufungua kesi, Mahakama Kuu ilitoa amri ya kuwataka polisi kutowaondoa wanakijiji hao kutoka shamba hilo la Arnold.

Wanakijiji hao wamekuwa wakiishi katika miliki hiyo kwa miaka 17, shukrani zikiiendea sera tata ya mageuzi ya ardhi ya Rais Mugabe, ambayo ilishuhudia wazalendo wakitumia nguvu kuwatimua wazungu kutoka mashamba yao.

Lakini inaonekana polisi wamepuuza amri ya mahakama ya kuzuia utekelezaji wa timua timua hiyo kwa manufaa ya mke wa rais.

Mwakilishi wa wanakijiji hao, ambao sasa hawana makazi, Innocent Dube, alikaririwa akisema wamelazimika kuwasilisha malalamiko yao SADC baada ya kuonekana hawawezi kupata msaada nchini hapa.

Waliwasilisha malalamiko hayo kupitia ubalozi wa Afrika Kusini nchini hapa kwa vile Swaziland, ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa SADC haina ubalozi.

"Waliweza kupokea shauri letu na mawasiliano yetu na kutuahidi kututafuta,” Dube alikaririwa akisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,227FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles