EU, AU zambariki Tshisekedi

0
620

Congo

Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU),wamesema  wameuzingatia uamuzi wa Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wa kumhalalisha rais mteule anayepingwa Felix Tshisekedi, wakiashiria wapo tayari kushirikiana nae kikazi.

Baada ya mkutano baina ya mawaziri wa Umoja wa Ulaya na Afrika, mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Federica Moghrini, amesema Tshisekedi, anakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kumaliza migawanyiko na kuunganisha taifa hilo la Afrika ya kati.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Richard Sezibera, ambaye alikuwa mwenyekiti mwenza wa mazungumzo amesema Umoja wa Afrika uko tayari kufanya kazi na watu wa Congo ili kumaliza changamoto zilizosalia wakati taifa hilo likifungua ukurasa mpya kisiasa.

Tshisekedi, anatarajiwa kuapishwa leo na kuwa rais mpya wa Taifa hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here