UDASA yaipiga mkwara serikali kuwalipa malimbikizo yao

0
786


Elizabeth Joachim Dar es salaam

Jumuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es saalam (Udasa) imeitaka Serikali kulipa malimbikizo ya zaidi ya Sh billioni 12 yanayodaiwa wanataaluma wa chuo hicho hadi ifikapo mwishoni mwa Februari.

Malimbikizo hayo ni posho ikiwamo ya nyumba ambayo ni zaidi ya Sh bilioni 6.272 ambalo ni deni la kuanzia Januari 2014 hadi Septemba mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Januari 23, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dk. George Kahangwa, amesema kwa kutofanya hivyo serikali itakuwa imeamua kuingia nao kwenye mgogoro.

“Inasikitisha baadhi ya watumishi wa Serikali kuchelewesha kwa muda mrefu malipo na sitahiki mbalimbali za wanataaluma kwa visingizio visivyoeleweka na ahadi zisizotekelezeka.

“Hii imekuwa kinyume cha utaratibu wa Serikali ya awamu hii ambayo imekuwa ikijaribu kuboresha maslahi ya watumishi. “Ni zaidi ya miaka mitatu sasa, wanataaluma wanaostahili kulipwa posho ya nyumba za kuishi wameendelea kudai stahiki hiyo bila mafanikio,” amesema Dk. Kahangw

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here