Tony Blair aomba marudio kura ya maoni Uingereza

0
868

Davos, Uswisi

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, amesema ipo haja ya marudio ya kura ya maoni kuhusiana na taifa hilo kujiondoa Umoja wa Ulaya.

Akiwa mjini Davos Uswisi, kunakofanyika kongamano la kiuchumi, Blair amesema kutokana na mgogoro wa bunge uliopo nchini kwake, jambo la busara ni kurejea kwa watu ili wafanye maamuzi.

Lakini pia amekosoa mipango yote ya Brexit ambayo inajadiliwa hivi sasa.

Aidha ameongeza kwamba ikiwa Uingereza, itasalia kwenye ushuru wa forodha au soko la pamoja la Umoja wa Ulaya, itakuwa na wajibu wa kufuata kanuni za Umoja huo na haitakuwa na usemi.

Blair, anaamini kama Uingereza, itajiondoa Umoja wa Ulaya (EU) bila ya makubaliano itakuwa ni janga kwa kila mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here