Lulu kufurahia Valentine Day na wenye uhitaji maalum

0
1214

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Muigizaji wa Filamu za Bongo, Elizabeth Michael (Lulu) amesema fedha atakazopata baada ya kuuza baadhi ya nguo zake atazipeleka kwa watu wenye mahitaji maalum ili wafurahia vyema siku ya wapendanao ‘Valentine Day’ inayoadhimishwa kila Februari 14.

Kabla ya kufikia uamuzi huo awali Lulu aliwataka mashabiki wake wachague kati ya nguo zake ambazowahi kuzivaa na angewagawia bure lakini ameamua kubadilisha zoezi hilo na kuziuza na fedha zake atazielekeza kwa watu hao weye uhitaji.

Lulu ametangaza hayo leo Jumanne Januari 23, kupitia ujumbe aliotuma katika ukurasa wake wa Insagram, ambapo anatumia kauli mbiu isemayo “Save my Valentine”.

“Kuelekea siku ya Wapendanao Februari 14, nimeamua kuuza sehemu ya nguo zangu ambazo yawezekana kuziona au hujaziona.

“Kisha pesa itakayopatikana kupitia mauzo hayo itaenda kusaidia watu wenye uhitaji muhimu katika jamii,” ameandika Lulu.

Aidha akijibu swali la mmoja wa shabiki aliyeuliza swali kuwa anaogopa kununua kwa sababu anahisi bei itakuwa ghali, Lulu amesema atauza bei ambayo watu wengi wataimudu na ikiwezekana nusu ya bei ambayo yeye amenunulia ili lengo alilokusudia lifanikiwe.LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here