“Eldorado” kutoka chechema hadi ‘nimekuwa’

0
1073

Na Elias Simon

Msanii wa kizazi kipya ndani ya mziki wa bongo fleva Tanzania, Elderado baada ya kushirikiana na Mr blue kupitia wimbo wa chechema kwa sasa ameachia wimbo mpya ambao amemshirikisha Christian bella katika wimbo wa ‘Nimekuwa’

Akizingumza na Papaso la Burudani jana, Elderado alisema Chechema ndio wimbo uliomtambulisha kwenye game ya bongo fleva kupitia Mr blue lakini wimbo huu mpya wa “Nimekuwa” amemshirikisha Christian bella.

“Chechema imefanya vizuri sana maana Mr blue ni msanii mkubwa ndani ya Tanzania lakini huu wimbo wa sasa ndio balaa tosha kupitia Christian Bella  maana Christian bella anajua sana sio msanii wa kawaida hapa nchini,” alisema Elderado.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here