28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mango aongoza Watanzania kumuaga Lowassa Dar

Na Esther Mnyika Mtanzania Digital

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango amesema maisha ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa yamewaachia mafunzo mengi ikiwemo uchapakazi hodari ndani ya chama na katika mambo binafsi hivyo wataendelea kumuenzi kwa kuchapa kazi.

Kauli hiyo ametoa Februari 13, 2024 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na Dk. Mpango wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Lowassa aliyefariki Februari 10, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na wengine.

Amesema alijitolea kutumikia Taifa kwa nguvu zake zote kwa nyazifa zote alizowahi kushika na jamii.

“Marehemu Lowassa amekuwa mtetezi hodari wa maslahi ya wananchi wake wa Jimbo la Monduli inatupasa kuiga mfano wake wa kutetea maslahi ya Taifa kwa utumishi wetu,” amesema Dk. Mpango. Amesema Lowassa alipenda sana familia yake hivyo wajifunze hilo kwa kuzipenda familia zao.

“Kuna mambo matatu enzi za uhai wake alisema kipaumbele chake cha kwanza elimu cha pili elimu na cha tatu elimu alikuwa anatambua sera ya elimu hadi akajenga shule za kata nchi nzima ni mchango wake katika elimu, tutamuenzi katika mambo mbalimbali, ” amesema Dk. Mpango.

Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema namna bora ya kumuenzi Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Lowassa ni kuendelea kuyaishi maono yake ya uzalendo, uwajibikaji ili iwe dira ya kuzidi kujenga umoja na kupiga hatua za maendeleo nchini.

“Nimejifunza mengi kutoka kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa ukiwemo uzalendo, uwajibikaji, ushirikiano na watu wa makundi yote na kuweka mbele maslahi ya nchi,” amesema Dk. Mwinyi.

Naye Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete amesema mengi yamekwisha semwa na viongozi wengine huku akitoa pole kwa mama Regna Lowassa kufuatia msiba huo ambao ni wa Taifa kwa ujumla .

“Ametoa mchango mkubwa kwa Taifa letu ameacha alama katika uongozi wake kikubwa ni kumuombea,” amesema.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Fedrick amesema Sumaye, kifo ni hatua ya mwisho kila mwanadamu ndo mwisho wake kifo
Jambo muhimu ni je? Uliacha je?

“Lowassa amefanyaMengi,katika jamii ya watanzania katika ngazi ya jamii watamkumbuka kwa maisha yake ameishi kwa kuchapa kazi nankutumikia Taifa,”amesema Sumaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles