26.1 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Lwaitama ataka wapinzani kuungana uchaguzi 2024/25

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Azavel Lwaitama ameshauri vyama vya upinzani kuungana ili kuwe na upinzani wenye nguvu kuelelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Dk. Lwaitama alikuwa akizungumza Machi Mosi,2024 wakati wa mkutano mkuu wa Ngome ya Wazee ya Chama cha ACT Wazalendo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Azavel Lwaitama, akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Ngome ya Wazee ya Chama cha ACT Wazalendo.

“Uchaguzi wa 2015 ni kielelezo kwamba lazima kuwepo muungano hasa kwa watu wenye utamaduni wa kushindanisha hoja ambao wanasukumwa na malengo ya pamoja…tupunguze mihemko kama kuna tofauti kaeni chini mzungumze,” amesema Dk. Lwaitama.

Dk. Lwaitama ambaye ni mwanazuoni pia ameshauri vyama vipya viachwe visajiliwe kwani wapigakura ndio watakaoamua aina ya chama wanachokitaka.

“Vyama 19 havitoshi waache wenye vigezo wasajili wapigakura wenyewe ndiyo watachuja. Uingereza, Marekani vyama vipo vingi lakini vinavyoshinda ni viwili tu,” amesema.

Mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo, Juma Sanani, akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa Ngome ya Wazee ya chama hicho.

Naye Kamishna Msaidizi Mwandamizi mstaafu wa Jeshi la Polisi, Jamal Rwambo, amesema tatizo la rushwa katika baadhi ya vyama limesababisha watu ambao wanafaa kuwa viongozi kushindwa kuchaguliwa

“Sasa hivi lipo tatizo la kimfumo katika vyama vya siasa, mfumo wa rushwa, kama ninyi mtaikataa kwa vitendo katika uchaguzi wenu mtakuwa mmelisaidia sana taifa.

“Msikubali kuingiza mfumo wa rushwa katika chama chenu kwa sababu umewaweka pembeni watu ambao wangeweza kusaidia nafasi mbalimbali kwenye chama, wapeni nafasi ya kuongoza watu wenye sifa…kiongozi bora anayeweza kubadilisha ngome ya wazee ni mkweli na ambaye si muongo,” amesema Rwambo.

Mshauri wa chama hicho, Juma Sanani, amesema uongozi ni utumishi na si fursa ya watu kufanya masilahi yao binafsi na kuwataka wazee hao kufanya uchaguzi kwa utulivu na nidhamu ili uchaguzi huo uwe bora kwa viwango vinavyokubalika kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles