27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wanahabari wapigana vijembe kisa kitita cha Ramadhan Cup

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kuelekea michuano ya Silent Ocean Ramadhan Cup, Wanahabari wanaounda timu za soka za Online Media na Mainstream Media, wametupiana vijembe kila upande ukitamba kuibuka na ushindi katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo ambayo bingwa ataondoka na kitita cha fedha zaidi ya Sh 5,000,000.

Michuano hiyo inatarajia kuanza Machi 12, 2024, ambapo timu hizo mbili zenye upinzani mkubwa zitakutana katika mechi ya ufunguzi kwenye viwanja vya JMK Park, jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Machi 4, 2024, Kocha wa Mainstream Media, Ally Kamwe na Kocha wa Online Media, Karim Boimanda, kila mmoja ametambia ubora wa kikosi chake na mbinu watakazotumia kuwafunga wapinzani.

Kamwe amerusha dongo kwa Online Media kuwa ni kikosi kinachoundwa na wanahabari wenzao ambao ni wasaliti waliojikusanya na kuanzisha timu ili washindane nao, hivyo wamejipanga kuwaonesha kazi na kuwaadhibu kama wasaliti.

“Mwaka huu kwenye timu ya wanahabari wameibuka wasaliti ambao ni viburi, jeuri ambao wanajiita Online Media, hawa wameibuka na kujiona wanaweza kujitegemea. Sasa niwaambie wadogo zangu Online chaka mliloingia sio,” ametamba Kamwe.

Hata hivyo ameishukuru kampuni ya Silent Ocean kwa udhamini wa mashindano hayo kwa msimu wa pili sasa kwani wameyapa thamani na kuyafanya yawe ya ushindani na kuondoa malalamiko.

    Naye Kocha wa Online Media, Boimanda amesema maneno yote na jumbe za vitisho wanazotumiwa haziwatii hofu, bali wanachohitaji ni kushinda na kuchukua ubingwa wa mashindano hayo na anafahamu wapinzani wao wanawahofia.

    “Sisi tunataka mechi, hatutaki siasa. Jumbe za simu za vitisho zinatumwa lakini ukiangalia ni msingi wa yote ni hofu kwa sababu wanajua mimi ni mchora ramani na ninawajua vizuri wanahabari ndio sababu walivyosikia nimekuja huku online wamestuka,” ametamba Bomanda.

    Kwa upande wake Ofisa Habari wa Silent Ocean Ramadhan Cup, Hassan Ahmed amesema tayari makundi ya michuano hiyo yenye timu 20 yamepangwa na bingwa atachukua zaidi Sh 5,000,000.

    - Advertisement -

    Related Articles

    LEAVE A REPLY

    Please enter your comment!
    Please enter your name here

    Stay Connected

    90,904FansLike
    214,997FollowersFollow
    586,000SubscribersSubscribe

    Latest Articles