27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aungwa mkono kutangaza tiba utalii

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Kampuni ya Vertex Group Experts inaunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza tiba utalii kwa nchi za Afrika ili waweze kuwafikia wagonjwa wengi na kuongeza pato la Taifa.

Akizungumza Machi 4, 2024 jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Herbert Swai amesema lengo lao kutoa huduma za tiba utalii kwa kuwaunganisha wagonjwa hospitali za nchini.

Amesema kampuni hiyo tangu kuanzishwa ina miaka miwili ikiwa mikakati yao ni kuendelea kukuza utaratibu huo ili wagonjwa wanaokuja kutibiwa watangaze nchi kutokana na huduma nzuri walizopata.

“Tunataka kuondoa dhana iliyojengeka kwa watu kuwa kutibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ni gharama kubwa hapana tuta hakikisha wagonjwa wa nje na ndani wanapata huduma bora na kwa gharama nafuu,”amesema Swai.

Amesema Rais Dk. Samia katambulisha Tanzania katika Afrika Mashariki ni kitovu cha huduma bora za afya lazima wafanye kazi ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa nje wanaokuja kutibiwa nchini.

Swai amesema kwa takwimu zao mwaka 2023 walipokea wagonjwa 47 kutoka nchi mbalimbali walitibiwa nchini katika Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Aidha amesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya wagonjwa wanakuja kutibiwa wengine wanakuwa hawajui lugha, kiswahili wala kingereza wanaongea lugha zao hivyo wanawakalimani kwa ajili ya wagonjwa wa nje ya nchi.

Ameongeza kuwa tiba utalii inawahusu watanzania wote na wapo kwa ajili ya kuwahudumia na kuwasiidia kupata huduma kwa haraka na wapo kisheria wanatambulika.

Mmoja wa wagonjwa kutoka visiwa vya Comoro waliopata huduma ya kutibiwa kupitia kampuni hiyo, Mohamed Abdulla amesema wanaishukuru imewawezesha kupata huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wanaendelea vizuri.

“Tunaahaidi kuwa mabalozi wazuri na kuwashauri wananchi wa Comoro kutibiwa Tanzania kwa sababu kuna huduma nzuri kama hauna ndugu wa kukusaidia kuna kampuni ambayo inasimamia kuanzia matibabu yako hadi mwisho,”amesema Abdulla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles