30.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Zuchu yamkuta Zanzibar, afungiwa miezi sita

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, ( BASSFU), limemfungia msanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Masoud maarufu kwa jina la Zuchu kuendesha shughuli zozote  za sanaa visiwani Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita.

Pamoja na adhabu hiyo,  pia BASSFU limepiga marufuku redio na televisheni za visiwani humo kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini  kwake Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B’,  Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Omar Abdalla Adam amesema hatua hiyo imekuja baada ya tukio la hivi  la Zuchu kutoa matamshi na kuonesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya Kinzanzibari akiwa jukwaani kwenye tamasha la Full Moon Party.

Amesema kwa mujibu wa kifungu namba  8 (1),(d) cha sheria nambari 7 ya 2015 ya Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, lina haki ya kumfungia msanii huyo kutokana na kukiuka sheria zilizowekwa za kuimba nyimbo zinazozingatia mila silka na Utamaduni wa Mzanzibari.

 Katibu huyo amefahamisha kuwa msanii huyo hana usajili  kwa hapa Zanzibar katika utendaji  wa kazi zake na wala hana mashirikiano ya aina yeyote katika Baraza hilo hivyo Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar limemfungia Msanii huyo na kumtaka kufika Zanzibar  kuomba radhi na endapo atakwenda kinyume na agizo hilo hatua kali  zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha Katibu ameitaka jamii ya Kizanzibar kupuuuza na kutosikiza nyimbo za msanii huyo  pamoja na kundi lake kwani kuendelea kuzisikiliza na kuimba nyimbo hizo ni kuharibu mila na utamaduni uliopo.

Nae Mrajisi wa Baraza hilo Juma Chuom Juma amesema  kwa mujibu wa Ibara namba 8 (B) inalitaka Baraza kuchukua hatua  kwa  wasanii wanaokuja  kuimba Zanzibar bila ya kufuata utaratibu uliyopo  kwani kuna sheria na utamaduni wake hasa ukizingatia kwamba  kipindi kinachokuja cha mwezi mtukufu wa Ramadhan.




- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles