30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia kuanza kusikiliza kero za wananchi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza kukutana na kusikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja ambapo atatenga siku moja kila mwezi kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

Lengo la kufanya hivyo ni kumuenzi kwa vitendo Rais Mstaafu Hayat Ali Hassan Mwinyi ambae alikuwa akifanya hivyo kipindi cha uongozi wake lakini pia kujua utendaji kazi wa watendaji wake katika kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa leo Machi 5, 2024, jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda wakati akitoa taarifa fupi kuhusu ziara yake katika mikoa 23 ya Tanzania Bara.

“Rais amepanga kutenga siku moja kwa kila mwezi ili kuwasikiliza wananchi wake bila kujali itikadi, dini wala ukabila, sasa hapa nitumie salamu kwa watumishi ambao wananchi walishaleta kero zao na hukuzitatua aje azifikieshe kwa Rais hapo kiama kitakua mlangoni kwako,”amesema Makonda.

Akizungumzia kuhusu ziara yake amesema kuna mambo mbalimbali yaliyobainika kwenye ziara hiyo ambayo yatakabidhiwa kwa katibu mkuu wa chama hicho ambapo mengine yalishughulikiwa hapo hapo.

Amesema kati ya mambo yaliyobainika ni dhuruma kwani watanzania wengi wameumizwa nazo, huku zikigawanyikwa kwenye mambo mengi.

“Sisi kama chama tunajukumu la kuishauri serikali ili kupambana na dhuruma hiyo ili kuwasaidia wananchi,”amesema.

Ametaja maeneo ambayo changamoto hiyo kwa kiashi kikubwa kuwa ni ardhi, wananchi wengi wamedhurumiwa ambapo walimwambia waziri wa ardhi kwenda kushughulikia na tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kutoa funzo kwa watu wanaotumia pesa kutapeli ardhi za waonyonge.

Amesema waziri anapaswa kufanya mapitio kwa watendaji wote ambao wameweka minyororo ya utapeli wa ardhi aweze kuwachukulia hatua kwani utapeli wa ardhi umeonekana kuwa na mtandao mpana na si wa mtu mmoja pekee.

“Kazi anayoifanya waziri wetu wa ardhi inapaswa kuungwa mkono na watendaji wote na wale wanaohusika na utapeli wachukuliwe hatua ili kukata minyororo hiyo ya utapeli”amesema.

Ameongeza kuwa kila mtendaji ambae amekuwa katika mnyororo wa kuwaonea wananchi abainishwe na kuchukuliwa hatua stahiki ili kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa zipo dhuruma nyingi zilizofanyika hasa za watu kujipatia mali kiudanganyifu hivyo mamlaka husiki zinapaswa kuchukua hatua ili kukomesha dhuruma hizo.

Amesema tatizo lingine ni viongozi kutokutatua kero za wananchi ambazo huwa wanazisikiliza hivyo chama kinaelekeza kila alie na nafasi anapaswa kutatua kero za wananchi kwani ofisi aliyopo ni ya umma, hivyo kutokutatua kero zao ni kinyume na utumishi.

“Viongozi tusitatue changamoto za wananchi kwa sababu ya kujuana bali tutatue changamoto kwani wanahaki na nchi yao na kupata haki,”ameongeza.

Aidha changamoto nyingine waliokutana nayo ni ukatili wa kijinsia ambao umejitokeza kwenye baadhi ya mikoa hivyo na inashughulikiwa ili kuja mkakati thabiti wa kuzuia ukatili huo.

Vilevile amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kuwapongeza viongozi wote wa chama walioshirikiana naye kwenye mikoa yao wakiwemo wenyeviti,wa NEC na wengine ambapo kazi hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa ilani ya chama ndani na nje ya chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles