29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Kalemani amtaka mkandarasi atumie vijana kukamilisha mradi wa Umeme Lindi

HADIJA OMARY, LINDI
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amemtaka mkandarasi anayesimamia mradi wa kusambaza umeme vijijini REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza State Grid, aongeze magenge ya vijana watakaofanya kazi hiyo ili ifikapo Desemba mwaka huu awe amemaliza na wananchi wawe na umeme.

Kalemani amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Lindi Mkoani humo wakati alipofanya ziara ya siku moja kukagua miundombinu ya umeme, maendeleo ya utekelezwaji wake pamoja na kuwasha umeme katika vijiji vilivyofikiwa na mradi huo.

Akizungumza na wananchi hao baada ya kufanya zoezi la kuwasha umeme katika shule ya Sekondari Chinogwe, ofisi ya Kijiji cha Ruponda pamoja na shule ya Sekondari Namangale amesema bado hajaridhishwa na kasi anayoendana nayo kwa mkandarasi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya meneja wa Tanesco Mkoa huo wa Lindi, Felisian Makota, katika mradi huo jumla ya vijiji 34 vinatarajia kufikiwa ambapo mpaka sasa jumla ya vijiji 18 vimeshawasha.

Naye Mkurugenzi Kampuni ya State Grid, Charles Mlawa amedai mradi huo ulikwama kutokana na changamoto ya nguzo hata hivyo ameahidi kufanyia kazi dosari zilizojitokeza kwani tayari wameshapata nguzo za kutosha kwa ajili ya shuguli hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles