31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara yatenga billioni 1.5 kwa ajili ya ukarabati wa soko

Ramadhan Hassan,Dodoma

Wizara ya Mfugo na Uvuvi imesema imetenga sh.bilioni 1.5 kwa ajili ya kukarabati soko la feri la Jijini Dar es salaam.

Hayo yameelezwa leo Mei 22 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati akihitimisha mjadala wa Wizara hiyo kwa mwaka 2018-2019.

Ulega amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kufanya ukarabati na soko la Feri.

Pia Ulega amesema Serikali imefanikiwa kuzuia uvuvi haramu katika eneo la Pwani.

“Uvuvi haramu ulikuwa umekidhiri lakini kwa sasa hakuna bomu linalopigwa na Watanzania wa upande wa Pwani wameanza kusahau,”amesema ulega.

Waziri Ulega amesema Wizara yake inatarajiwa kupata sh.bilioni 4 kwa ajili ya kununua meli ambayo itasimamiwa na Shirika la Uvuvi la Taifa (TAFICO), “Ndio tunaenda kusimamia Tafico kuna mama mmoja mahiri atasimamia hili, tuna uhakika wa kupata bilioni 4 kwa ajili ya kununua meli,tunafanya hivyo ili tuionyeshe dunia watu walikata tama kwamba kwetu hakuna samaki.

“Sisi tumengeneza mkakati wa kisasa kwa kuingia mikataba na tutaenda kujenga bandari ya uvuvi.

Ulega amesema kwa sasa kumekuwa na Pweza wengi kutokana na kudhibiti mazalia yao katika eneo la Kilwa.

“Maeneo ya mazalia pale Kilwa tumedhibiti sasa Pweza wanapatikana na sasa wanapata mazao ya kutosha hiyo ni kazi yetu sisi.

“Naomba niwahakishie Wabunge kazi inaendelea na sisi hatutarudi nyuma sisi kama wanadamu maoni yenu tutayafanyia kazi,”amesema Ulega.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles