24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

Nyota nane Yanga kuikosa Mbeya City, U20 kuokoa Jahazi

NA LULU RINGO, DAR ES SALAAM

Wachezaji nyota nane wa kikosi cha kwanza cha Yanga, wataikosa mechi ya leo Mei 22 ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City kutokana na kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Mei 22, Mratibu wa klabu ya Yanga, Hafidhi Salehe amewataja wachezaji hao kuwa ni Ibrahim Ajib, Mrisho Ngasa, Andrew Vicent, Juma Makapu, Juma Abdul, Mohamed Banka, Gadiel Michael na Paul Godfrey.

“Katika mchezo wa leo tutawakosa wachezaji wetu muhimu wa kikosi cha kwanza wengi wao wanasumbuliwa na homa isipokuwa Gadiel Michael na Mohamed Banka ambao ni majeruhi,” amefafanua Hafidhi.

Licha ya wachezaji hao kukosekana mratibu huyo ameweka wazi kuwa watalazimika kuwatumia wachezaji wa timu ya vijana chini ya miaka 20 (U20) ambao watashirikiana na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza katika mchezo huo.

“Kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa kutoka kikosi cha kwanza tutalazimika kuwatumia vijana wetu wa U20 ambao ni Shabani Mohamed (mshambuliaji) na Omary Bakari (beki) watakao jumuika na wengine wa kikosi A,” amesema mratibu huyo.

Yanga itashuka katika dimba la Uhuru leo kuvaana na timu ya Mbeya City kutoka Mbeya ikiwa na alama 83 chini ya mahasimu wao Simba wenye alama 91 ambao jana wametangaza kuwa mabingwa wapya wa msimu wa 2018/19 baada ya kuinyuka Singiga United bao 2-0 na kusaliwa na michezo miwili mkononi sawa na Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,222FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles