24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kigamboni yatoa milioni 400 kusaidia wajasiriamali

Mwandishi wetu

Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni imetoa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 400 kwa vikundi 128 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi awamu ya pili ya mikopo hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ng’wilabuzu Ludigija, amesema kwa mwaka 2018/2019 walipanga kutoa mikopo ya Sh milioni 537.1.

Amesema katika awamu ya kwanza zilitolewa Sh milioni 250 kwa vikudi 97 na awamu ya pili zimetolewa Sh milioni 150 kwa vikundi 31.

“Kwa kuzingatia sera na maelekezo ya Serikali tumekuwa tukitenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kuyawezesha makundi haya.

“Walionufaika wahakikishe wanarejesha fedha hizi kwa wakati ili kujitengenezea nafasi ya kupata mikopo mingine,” amesema Ludigija.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa ya mapato katika halmashauri hiyo kutoka Sh bilioni 3 hadi kufikia Sh bilioni 6 hatua iliyowezesha kuongezeka kwa vikundi vinavyopatiwa mikopo.

“Tulipotoa awamu ya kwanza ya mikopo hakukuwa na vijana waliojitokeza fedha zote walikabidhiwa kinamama na wenye ulemavu. Je, vijana wenzangu mnakwama wapi?

“Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo, changamkieni fursa hizi mjikwamue kiuchumi,” amesema Sara.

Kati ya vikundi 128 vikundi 92 ni vya wanawake, 28 vya vijana na vinane vya watu wenye ulemavu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles