24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Bashiru: Mvitathmini vyama vya siasa

Mwandishi wetu -Zanzibar

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amewataka wananchi kuvifanyia tathmini ya kina vyama vya siasa vyenye usajili na vinavyopokea ruzuku kisha kuchagua chama chenye sifa na vigezo vya kuongoza nchi.

Ushauri huo alitoa jana wakati akizungumza na wana CCM na viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema watanzania wanahitaji chama chenye nguvu, kitakachosimamia rasilimali za nchi, kitakacholinda mipaka ya nchi, kitakacholinda Mapinduzi, Muungano na Uhuru kama kinavyofanya CCM.

“Vyama vya upinzani vya Tanzania sio madhubuti na havina uwezo wa kushindana na CCM kwani havipo karibu na wananchi vimekuwa vikiibuka wakati wa uchaguzi bila kuwa na sera wala muelekeo wa kiushindani katika medali za kisiasa. CCM imejipambanua katika kuwahudumia wananchi kama kilivyoahidi katika kampeni zake zilizopita,”  alisema Dk. Bashiru

Kutokana na hali hiyo, Dk. Bashiru, alisema  chama hicho kimetengeneza fomu milioni moja kwa ajili ya uchaguzi wa ndani kuwashindanisha wana CCM kwa lengo la kupata wagombe bora na wenye sifa.

“Upinzani waseme wao wamepitia mchakato upi kuwapata wagombea wao waonadai wameenguliwa kwa kuonewa CCM ndiyo chama pekee nchini Tanzania chenye kufuata na kutoa demokrasia kuliko vyama vyengine vyote vya upinzani,” alisema

Mtendaji Mkuu huyo wa CCM alisema kuwa tafsiri ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa inatoa picha kuwa chama hicho kuwa kitashinda kwa ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles