29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Mkemia Mkuu kuanzisha kanzidata ya DNA

Aveline Kitomary , Dar es salaam

MAMLAKA ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatarajia kuanzisha  mfumo wa kanzidata  wa Taifa katika upimaji wa sampuli za vinasaba (DNA), utakaosaidia kurahisisha utambuzi wa miili iliyoharibika na watu wanaojihusisha uhalifu kwa kurahisisha uchunguzi  na kutokutumia ndugu.

Mfumo huo pia utatumiwa katika kurahisisha huduma za matibabu  kwa kuangali mfanano wa vinasaba unaolingana kwa ndugu wa karibu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, wakati akitoa tathimini ya miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Mgufuli, Mkemia Mkuu wa Serikali Dk.  Fidelice Mafumiko, alisema kuwa mfumo huo pia utatumika  kwa watoto wa mtaani ambao wametelekezwa na wazazi wao.

“Tunataka tutumie kipindi cha miaka miwili kwamba hilo suala likamilike hilo linaenda hatua kwa hatua na inahitaji umakini mkubwa ambapo tuitashirikiana na taasisi zingine kama NIDA na RITA  mfumo huo utasaidia  utambuzi katika miili iliyoharibika.

“Lakini hii ni tofauti ukiwa na database badala ya kutafuta ndugu tunawapata  kupitia mfumo huo  pia itasaidia sana kwenye uhalifu mfano ubakaji ,mauaji ya kutumia silaha sasa tunapoanza kutumia  mfumo wa database tutaweza kuwatambua.

“Pia itatumika katika matibabu tutashirikiana na madaktari katika kuwasaidia kugundua DNA ambazo zinafanana mfano mtu akitaka kumtolea ndugu yake figo mfumo utaonesha nani ana uhusiano na anastahili ampatie mgonjwa figo kati ya ndugu,” alisema.

Alisema faida nyingine ya mfumo huo pia utahusika katika suala zima la mirathi na  uhalifu wa makosa ya jinai kama wizi, ubakaji, mauaji na majanga.

Alibainishha kuwa mfumo huo utaanza kwa watoto ambao wanazaliwa,katika mifumo ya matibabu na mahakamani.

Akielezea mafanikio waliyopata kwa miaka mine alisema tayari wameshafanya uwekezaji katika miundombinu ya maabara za uchunguzi  ikiwamo vifaa na majengo.

“Tumenunua mitambo yenye thamani ya bill 6.5 hizi ni mashine za kisasa za upimaji wa DNA  9 mpya, pia matumizi ya Tehama yameimarika kama matumnizi ya mfumo wa elektroniki, mifumo ya usajili wa wadau wa kemikali kwa njia ya mtandao, mfumo wa usimamizi wa fedha kuna malipo ya serikali na hata majengo tumejipanua tuko ukanda wa mikoa sita nchini,” alisema

Aidha alisema kuwa kwa kipindi cha miaka minne mapato ya mamlaka yameongezeka  kutoka Sh bilioni 9.342 mwaka 2015 na 2016 na kufikia Sh bilioni 24.246 kwa mwaka 2018 hadi 2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,905FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles