24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DC Nyamagana: Wanawake changamkieni fursa zninazoletwa na NMB

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Bi Amina Makilagi amewaasa wanawake wilayani humo kuchangamkia fursa zinazoletwa kwao na benki ya NMB kwa maendeleo yao yakiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na umati wa wanawake na wakazi wengine wa mkoa huo waliohudhuria uzinduzi wa klabu ya ‘mwanamke jasiri’ mkoani Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.

Makilagi alisema kuwa wakazi wa Mwanza wasiache kuchangamikia fursa zinazoletwa na benki ya NMB kwani benki hiyo ina malengo mazuri ya kutaka kuleta maendeleo kwa wateja wake na ndio maana imejikita katika ubunifu wa huduma mbalilmbali zenye kuleta manufaa makubwa kwa wateja wake na Taifa kwa ujumla.

“Benki ya NMB ina malengo mazuri sana kwenu na ndio maana kila mara wamekuja na huduma mpya, nzuri na zenye manufaa kwa wateja wao na kwa maslahi makubwa ya taifa kwa ujumla. Kama fursa zote hizi zinaletwa kwenu, zichangamkieni basi nanyi mkanufaike na muendelee kiuchumi,” alisema Makilagi.

Aidha, mkuu huyo wa wilaya aliwasihi sana wanawake kutoogopa kuchukua mikopo ya NMB kwni ni mikopo Rafiki sana na masharti yake sio magumu kabisa. Aliwasisitiza kuwa fursa za biashara katika wilaya ya Nyamagana na mkoa wa Mwanza kwa ujumla ni nyingi na kwa utaratibu mzuri wa mikopo kutoka benki ya NMB, kilio cha mitaji kimepata ufumbuzi.

Amina Makilagi ambae awali alikuwa mbunge wa viti maalum alisema; “Jitahidini kuchukua mikopo kutoka NMB mkajiendeleze zaidi, mikopo yao ni nafuu na masharti yao sio magumu kabisa. Kwa fursa za biashara zilizopo Mwanza na hii mikopo ya NMB hamna kisingizio tena cha kutokuwa na mitaji,” amesema.

Akizungumza katika uzinduzi huo, mkuu wa kitengo cha biashara kutoka benki ya NMB Alex Mgeni alisema lengo la kuzindua klabu hii ni kuzidi kumpa ujasiri mwanamke na wao kama benki kupata fursa ya kutoa mafunzo ya fedha kwa wanawake ilikuwaongoza vyema katika ukuaji wao kiuchumi. 

”Tunazindua rasmi klabu ya “Jasiri” kwa mkoa wa Mwanza, na lengo kuu ni kuhakikisha tunawezesha wanawake kwa kuwapatia mafunzo na pia kuonesha fursa ambazo NMB imewaletea ili kuweza kufikia malengo yao’,” amesema Alex Mgeni.

Alex aliongeza kuwa ndani ya mwaka mmoja, benki hiyo imefanikiwa kutoa mikopo ya bilioni 100 kwa wanawake Zaidi ya 8000 mkoani Mwanza huku akiwakaribisha wateja wengine kufika ili kujipatia mikopo kwa manufaa yao.

Uzinduzi huo uliudhuriwa na wateja na wafanyabiashara wa benki ya NMB yenye matawi ya Igoma, Ilemela, Buzuruga, Mwanza Business Centre, Kenyatta, Rock city na Pamba jijini Mwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles