DC Nkasi awakutanisha wasomi, waanzisha Kiwanda cha Chaki

Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Saidi Mtanda, amewaunganisha pamoja vijana wasomi ambao wamefanikiwa kuanzisha kiwanda cha kutengeneza chaki cha Nkasi Chalks.

Mtanda amesema wazo la kuanzisha kiwanda cha chaki alilipata baada ya kuvutiwa na wazo la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka la kuwa na kiwanda kama hicho mkoani kwake.

“Nilivutiwa sana na wazo la Mtaka kuwa na kiwanda cha chaki. Nilichofanya nimewaunganisha vijana sita wenye shahada za vyuo mbalimbali na kuanzisha kikundi ‘Nkasi Intellectuals’.

“Vijana hapo tumewapatia ofisi na mkopo wa Sh millioni nane na tayari wameanza kuzalisha chaki kwa matumizi ya shule zetu 130 za Wilaya ya Nkasi,” amesema Mtanda.

Pamoja na mambo mengine, Mtanda amesema kwa mwezi watakuwa na uwezo wa kuuza boksi 500 za chaki kwa Sh 2,500.

Mkuu huyo wa Wilaya pia amemshukuru Mtaka kwa wazo hilo huku akimuita mwalimu wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here