28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

TEF kutangaza washiriki mafunzo ya ujasiriamali mwaka huu

Lagos, Nigeria
Taasisi ya Hisani la Tony Elumelu Foundation (TEF), ambayo inaongoza kwa uwezeshaji wajasiriamali wa Afrika, inatarajia kutangaza washiriki waliopitishwa katika programu ya ujasiriamali Machi 22, mwaka huu.

Akizungumzia programu hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa TEF, Ifeyinwa Ugochukwu, ambaye anachukua nafasi ya Parminder Vir, atakayebakia katika bodi ya ushauri kuanzia Aprili Mosi, mwaka huu, amesema kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya wanufaika wa kila mwaka kutoka 1,000 ya sasa.

“Kila mwaka tunashuhudia ongezeko la waombaji hivyo idadi ya wanufaika itapaswa kuongezeka. Mbia wetu, Accenture Development Partnerships, kwa sasa anatathimini na kupitisha waombaji.

“Zaidi ya wajasiliamali 215,000 wa Afrika kutoka mataifa 54 waliwasilisha maombi likiwa ongezeko kutoka waombaji 151,000 wa mwaka jana na kutoka 62,000 mwaka jana hadi 90,000 mwaka huu kwa upande wa wanawake,” amesema.

Amesema kupanda kwa takwimu hizi kunaonesha dhamira ya mjasiriamali wa Afrika kuendeleza bara letu na wanatakiwa kugeuza dhamira hii kuwa fursa ya biashara itakayochochea maendeleo.
Kila mwaka TEF hukaribisha maombi ya uwezeshaji kwa wajasiriamali wa Afrika, wenye biashara zenye umri usiozidi miaka mitatu.

Kupitia programu hiyo yenye thamani ya Dola milioni 100, taasisi hiyo huwezesha wajasiriamali 1,000 kila mwaka, ambao hupokea Dola 5,000 kama mtaji wa kuchochea biashara zao.

Aidha hukutana na wataalamu, programu ya mafunzo ya wiki 12 na fursa za kutangaza biashara zao kwa ulimwengu wa kibiashara.
Waombaji wote hupata fursa ya kuunganishwa na mtandao wa kidijitali wa TEFConnect, ambao ni kitovu cha wajasiriamali barani Afrika, ukitoa fursa ya kuunganishwa na mitandao, mafunzo na vyanzo zaidi vya mitaji na fursa za kibiashara.

Katika miaka mitano tangu taasisi hiyo izindue programu ya ujasiriamali, imewezesha moja kwa moja wajasiliamali 4,000 wa Afrika na wengine 470 wakisaidiwa na wabia wa TEF.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles