23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Msajili awacharukia wanachama CUF wanaochoma bendera

Elizabeth Joachim, Dar es Salaam

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amekemea kitendo cha kuchoma moto bendera ya Chama cha Wananchi (CUF), kilichofanywa na waliokuwa wanachama wa chama hicho baada ya kuhamia Chama cha ACT-Wazalendo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jaji Mutungi leo Jumanne Machi 19, imesema kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria.

“Kifungu cha 11c cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 kinakataza mwanachama au kiongozi yeyote wa chama cha siasa kufanya kitendo chochote kinachodhihaki bendera ya chama kingine na adhabu ya kosa hilo ni faini isiyozidi Sh milioni moja au kifungo kisichozidi miezi sita au adhabu zote.

“Katika mitandao ya kijamii kuna video inaonesha watu wakipandisha bendera ya ACT-Wazalendo kwa kutumia tamko takatifu la Dini ya Kiislamu (Takbir), kitendo hiki si tu dhihaka bali pia ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi hususani Sheria za Vyama vya Siasa,” imesema taarifa hiyo.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Mutungi amesema jambo hili linafanyiwa kazi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kwani kifungu cha 9 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, kinakataza chama cha siasa kutumia dini kufikia malengo yake.
Aidha, amewaasa wanachama na mashabiki wote wa vyama vya siasa kuepuka na kujishusha na vitendo vyote vya uvunjifu wa sheria kwani wakifanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria binafsi na chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles