30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

DC MNYETI AELEZA SABABU ZA KULIVIMBIA  BUNGE

Na MWANDISHI WETU-ARUSHA


KAULI ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti akidai wale wanaofurahia taarifa za yeye kuitwa, kuhojiwa mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, wanajisumbua.

Alitoa kauli hiyo wilayani hapa juzi akiwa kwenye kikao cha watendaji wa Halmashauri Wilaya ya Arumeru wakiwamo wenyeviti wa vijiji, watendaji na madiwani.

Kauli hiyo ya Mnyeti inatajwa kuwa ni ujumbe mzito na salamu kwa Bunge lililotoa uamuzi wa kuwaita viongozi wawili akiwamo yeye kuhojiwa juu ya kauli zao zinazodaiwa kulidhalilisha na kudharau hadhi ya Bunge.

“Na wala mtu asitumie muhimili mwingine kunyanyasa watendaji wa Serikali kama mtendaji wa Serikali amehusika kwenye kosa hatusemi asichukuliwe hatua.

“Lakini kama mtendaji anakwenda kunyanyasika hatutakubali tuko imara na tupo tayari kwa ajili ya mapambano hayo na nadhani hata nyinyi ni mashahidi kuna watu walitaka kumuita sehemu mtu fulani,” alisema Mnyeti.

“Unapohoji kuingilia mhimili wako wakati huo huo unaita muhimili usiokuhusu kwenda kuuhoji bado na wewe unaingilia muhimili mwingine, Arumeru Oyeee,” alisema Mnyetina na kuongeza:

“Kwa hiyo wale waliokuwa wameanza kufurahia habari hii, imekula kwao mimi nipo hapa Arumeru na kwa bahati nzuri kila aliyekuwa anasimama amenipa sifa nzuri sana lakini mimi nasema hizi si sifa zangu ni sifa zenu.

 

“Kamwe hatutaweza kuona mtendaji akienda kunyanyasika hatutakubali tuko imara na tupo tayari kwa mapambano hayo na nadhani hata nyinyi ni mashahidi kuna watu walitaka kumuita sehemu mtu fulani,” alisema.

Katika kikao hicho Mnyeti alitolea mifano ya baadhi ya mambo aliyodai yameanzia wilayani kwake na kuwa ya kitaifa likiwamo suala zima la dawa za kulevya kuwa lilianzia wilayani kwake na sasa limekuwa la kitaifa.

“Wengine wanasema wametukanwa kwenye mitandao kwamba wamesinzia, wamelala wana koroma bungeni. Lakini ukilala tusiseme kama umesinzia si umesinzia na sisi tumeona unasinzia na tumesema kwa hiyo mambo mengi yanaanzia Arumeru,” alisema Mnyeti.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Makiba Emmanuel Mollel aliyehudhuria kikao hicho akizungumzia suala la kuitwa na Bunge alisema, mkuu huyo wa wilaya alipaswa kutumia hekima nasi kufanya kejeli dhidi ya muhimili mwingine wa dola.

“Bunge na Serikali ni mihimili miwili ya dola inayojitegemea sasa anaposema sijui imekula kwao nadhani hiyo si heshima alipaswa kuitikia wito,” alisema Mollel.

Hivi karibuni bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wabunge walieleza namna walivyopokea taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Mnyeti wakilikashifu muhimili huo.

Makonda anadaiwa kutoa kauli za kulikashifu Bunge. “Zile ni mbwembwe tu, wale huwa wanachoka na kusinzia hivyo ni lazima wakati mwingine kuwe na watu akili zao zinasaidia kucheka,” alinukuliwa Mkonda.

Kwa upande wake Mnyeti  alituhumiwa kupitia sauti yake iliyorekodiwa kukashifu utendaji kazi wa Bunge na hivyo wabunge kwa pamoja walitoa maazimio kadhaa kuhusu viongozi hao wawili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles