25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Dawa tatu zapigwa marufuku

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imewataka watu wote waliokuwa wanatumia dawa za Raniplex 150 mg, Rantac 500mg/mL na Aciloc 150mg, ambazo hutumika kwa kiungulia na vidonda vya tumbo kuacha mara moja na kuripoti kituo chochote cha Afya kilicho karibu.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili kuhusiana na katazo hilo ambalo taarifa zake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Afisa habari wa Mamaka hiyo, Gaudencia Semwanza, alikiri kuwa taarifa hizo ni za kweli na kwamba wamefanya hivyo kwa ajili ya usalama.

“Ni kweli taarifa hizo zinazosambaa ni za kweli na tumefanya hivyo kwa ajili ya usalama tu, lakini pia taarifa kamili ipo kwenye tovuti yetu,” alisema Semwanza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyoko kwenye tovuti ya mamlaka hiyo, TMDA imefanya tathmini kamili ya dawa zote za binadamu zilizo na ‘ranitidine’ kama kingo hai ya dawa (API).

Ranitidine ni dawa inayotumiwa kwa dalili nyingi ikiwamo ya matibabu na kuzuia vidonda vya tumbo na matumbo, kudhibiti uzalishaji wa asidi ya tumbo kwenye utando wa moyo na vile vile matibabu ya ugonjwa wa gluro-esophageal Reflux (GERD). 

“Mapitio ya bidhaa zilizo na ranitidine ililenga kutambua yale ambayo yana N-nitrosodimethylamine (NDMA) – uchafu ambao umethibitishwa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa kansa unaoweza kusababisha mfano na saratani kwa binadamu.

“Hivyo kufuatia ukaguzi, bidhaa za dawa zilizoorodheshwa hapo chini zimezingatiwa ili kuangalia hali ya uzalishaji, lakini tulibaini kuwa zinazalisha uchafu,” ilieleza taarifa hiyo na kuziorodhesha dawa hizo kuwa ni.

Raniplex 150 mg inayozalishwa Cyprus, Rantac 500 mg/mL na Aciloc 150 mg zinazozalishwa nchini India.

TMDA ilisema kuwa kutokana na uchunguzi wake, imeamua kuzuia dawa hizo ili kulinda afya ya watumiaji.

“Kuhusiana na hili na kulinda afya ya umma, TMDA imesimamisha utumiaji wa bidhaa hizi za dawa kuanzia Novemba 15, 2019, pia watengenezaji wote wameelimishwa na kuamriwa kubadili muundo wao ikiwa ni pamoja na michakato ya utengenezaji ili kutengeneza bidhaa ambazo hazizalishi uchafu.

“Kama kuna bidhaa mbadala za dalili kama hizo kama Omeprazole, lansoprazole, Rabeprazole, Pantoprazole na Esomeprazole ambazo zimeidhinishwa kutumiwa na TMDA, wagonjwa wanashauriwa kushauriana na watoa huduma zao za afya kupata maagizo mapya kulingana na hali yao ya ugonjwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Pia imesema kuwa, wauzaji wote na wasambazaji wote wameelekezwa zaidi kuacha kusambaza au kuuza bidhaa zilizotajwa hapo juu kwa mtiririko huo na kutaarifu TMDA kwa mwongozo wa kukumbuka.

“Ikumbukwe kwamba kusimamishwa ni kwa bidhaa tatu zilizoorodheshwa hapo juu na kwamba bidhaa zingine zilizo na ranitidine za viwanda vingine hazijasimamishwa na zinaweza kutumika.

“Watumiaji bado wanakumbushwa kuwaarifu TMDA kuhusu athari yoyote mbaya ya dawa (ADR) ambayo inaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya dawa hizi au dawa zingine zozote kama sehemu ya mfumo wake wa maduka ya dawa,” imeeleza taaifa hiyo na kuhitimisha kuwa,

“Ikumbukwe pia kwamba kusimamishwa, kupiga marufuku na kukumbuka kwa bidhaa za ranitidine zilizo na uchafu N-nitrosodimethylamine kwa sasa zinaendelea katika nchi nyingine nyingi duniani,” ilisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles