23.6 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kusaka fursa za ajira kwenye lugha ya kichina

Na FARAJA MASINDE

SERIKALI imesema itaendelea kusaka fursa ya watanzania wengi kujifunza lugha ya kichina lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha ushirikiano ulipo baina ya nchi hizo mbili pamoja na fursa ya ajira kwa vijana.

Kauli hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha katika hafla ya utoaji tuzo ya Balozi kwa wanafunzi 80 wa kitanzania waliohitimu ngazi mbalimbali ya somo la lugha ya Kichina.

Alisema, kwa sasa China ni miongoni mwa mataifa yanayofanya vizuri kwenye eneo la uchumi na uwekezaji kwa ujumla ulimwenguni hivyo kuna haja kubwa ya vijana wa kitanzania kujifunza lugha hiyo.

“Wote mnafahamu kwamba kwa sasa ubalozi wa China na taasisi ya Confucius wanasaidia vyuo vinne na shule mbalimbali nchini kuhakikisha kuwa wanajifunza kichina jambo ambalo ni jema na serikali tunaliunga mkono.

“Kwani iko wazi kwamba China ni moja ya mataifa yanayoongoza uchumi na teknolojia, hivyo kwa vijana wetu kujifunza lugha hii kutawasaidi kupata fursa kubwa ya ajira ikizingatiwa kuwa tuko kwenye ujenzi wa viwanda hivyo itakuwa rahisi kwa wawekezaji wa kichina watakapokuja hapa kutoa ajira kwa vijana wetu,” alisema Ole Nasha

Aliongeza kuwa, dunia ya sasa ni ngumu kumweka mchina pembeni, hivyo kwa miaka mitatu  kuna wanafunzi zaidi 200 wameenda kusoma kwa msaada wa China jambo alilosema kuwa nilakupongezwa.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini, Wang Ke, alisema kumekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojifunza lugha ya kichina hapa nchini jambo ambalo alisema kuwa ni kuendelea kuimarika kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili.

“Kwa mwaka huu Serikali ya China imetoa nafasi 302 za ufadhili kwa wanafunzi wanaojifunza kozi mbalimbali nchini, lakini pia , hadi sasa wanafunzi 1,900 wamepata ufadhili wa Serikali ya China na kwenda kusoma nchini China miongoni mwao wamehitimu nchini China na wamerudi Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa taifa lao kwenye sekta mbalimbali hapa nchini,” alisema Wang Ke.

Naye mmoja wa wanaufaika wa mopango huo, Amos Benjamin, alisema ameweza kutumia fursa ya kujua kichina kwa kushiriki katika kambi ya ugunduzi kwa vijana duniani(UNLEASH) uliofanyika  Shenzhen ambapo aliibuka kidedea kwa kubuni teknolojia ya kulisha samaki.

Amesema Serikali ya China imekuwa nchi inayotoa idadi kubwa zaidi ya nafasi za Ufadhili kwa wanafunzi wa Tanzania.

Mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa China, Amos Benjamini, alishiriki katika iliyofanyika Shenzhen ambapo aliibuka kidedea kwa kubuni teknolojia ya kulisha Samaki.

Katika tuzo hizo wanafunzi 20 walipata tuzo bora na wengine 60 walipata tuzo ya mafanikio, wanafunzi hao ni kutoka  vyuo mbalimbali hapa nchini kikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles