29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Maporomoko ya udongo yaua watu 36 Kenya

NAIROBI, KENYA

MAOFISA nchini Kenya wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na tukio la maporomoko ya udongo katika eneo la Pokot magharibi mwa Kenya imefikia 36.

Hii ni baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo.

Maporomoko hayo yalioathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, yameripotiwa kusababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Vijiji hivyo vinasemekana kutenganishwa kabisa na mafuriko ambayo yameharibu daraja.

Maofisa pia wamesema kuwa miili ya watu 12, ikiwemo ya watoto saba ilipatikana jana asubuhi.

Joel Bulal, mmoja wa wasimamizi wa serikali katika eneo hilo ameliambia gazeti la Daily Nation kuwa shughuli za uokozi zinaendelea huku na kuwatafuta wale ambao hawajulikani waliko.

Kamishna wa jimbo hilo, Apollo Okelo amesema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na kuongeza kuwa shughuli ya kuwaokoa zinaathiriwana hali mbaya ya hewa.

“Tunajaribu kutafuta mahali ambapo daraja limesombwa na maji ya mafuriko,”alinukuliwa na mtando wa habari wa Standard nchini Kenya.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha miti iliyosombwa na maji na mingine kung’olewa, huku matope yakisambaa barabrani

Katika Twitter yake, Shirika la Msalaba mwekundu limethibitisha ripoti zinazoashiria tukio la maporomoko “makubwa” ya matope.

Maporomoko hayo yaliyoathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, yameshuhudia mvua nyingi katika eneo la Afrika Mashariki na upembe wa Afrika kwa wiki kadhaa sasa.

Nchini Sudan Kusini kijiji kizima kimesombwa na maji na ajali kadhaa zilizotokana na mvua zimeripotiwa Tanzania, Ethiopia na Somalia.

Wanasayansi wanasema hali mbaya ya hewa inatarajiwa kukumba baadhi ya nchi katika kanda hiyo kwasababu viwango vya joto katika Bahari Hindi vinatarajiwa kupanda kupita kiasi cha kawaida, hali ambayo huenda ikasababisha mvua kubwa .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles