26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyekuwa mlinzi wa Kagame jela maisha kwa kujaribu kumuua

KIGALI, RWANDA

MAHAKAMA ya Rufaa mjini Kigali imethibitisha hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Luteni Joel Mutabazi ambaye alikuwa mlinzi wa karibu wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Hatua hii imechukuliwa baada ya Mutabazi kukata rufaa kupinga hukumu hiyo aliyopewa mwaka 2014 baada ya kupatikana na hatia ya kutaka kuangusha serikali na kutaka kumuua Rais Kagame.

Kesi hiyo ilichukua muda mrefu kutokana na kwamba idadi ya wahusika walikuwa jumla watu 9 akiwemo Luteni Joel Mutabazi ambaye yeye mwenyewe alishtakiwa makosa nane.

Baada ya mahakama ya rufaa kuyachambua mashtaka hayo jinsi yalivyo kulingana na faili la mashtaka la kila mtu, imeamua kutoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kama ilivyotolewa mahakama kuu ya kijeshi dhidi ya Joel Mutabazi mwaka 2014.

Mahakama imesema kwamba kuna ushahidi wa kutosha wa kuhusika kwake kwa makosa makubwa ya kuhatarisha usalama wa taifa.

Mutabazi alikuwa akikana  kutaka kuiangusha serikali na alifanya ugaidi kwa kushirikiana na makundi ya waasi ambayo ni pamoja na RNC (Rwanda National Congres) linaloiongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda Jenerali Kayumba Nyamwasa na kundi la FDLR.

Alidaiwa kutaka kumuua Rais Kagame ili kufuta ushahidi kwamba ,Luteni Joel Mutabazi alisuka njama ya kulipua boti la Rais katika ziwa Muhazi karibu na makazi ya kiongozi huyo.

Mutabazi alikuwa mlinzi wa karibu wa rais Kagame akihusika na makazi ya rais yaliyoko katika ziwa Muhazi mashariki mwa Rwanda.

Hoja zake za kukata rufaa zilikuwa kwamba alizuiliwa kinyume na sheria, akisisitiza kwamba alitekwa nyara alipokuwa uhamishoni nchini Uganda.

Vilevile alihoji kuwa wakati anakamatwa hakuwa tena askari wa Rwanda je kuna haja gani kwa kesi yake kuendeshwa na mahakama kuu ya kijeshi.

Askari wengine 8 walioshtakiwa pamoja pia wamepewa hukumu ya vifungo kati ya miaka 10 na 25 isipokuwa mmoja tu Kalisa Innocent aliyepunguziwa adhabu na kupewa kifungo cha miaka 12 jela badala ya 25.

Mnamo Januari mwaka 2014, watu 16 nchini Rwanda walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupanga njama ya ugaidi.

Washitakiwa hao ni pamoja na  Mutabazi.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakielezea wasiwasi kuhusu tisho dhidi ya maisha ya wapinzani wa serikali ya Kagame.

Awali ofisa mmoja mkuu katika Umoja wa mataifa, alikosoa namna ambavyo serikali ya Rwanda inawatendea wanasiasa wa upinzani.

Inaelezwa baadhi yao walikamatwa na kufungwa jela kwa kile kilichosemekana kuwa kueneza uvumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles