Davido ashangazwa na Chioma

0
1435

LAGOS, NIGERIA 

STAA wa muziki nchini Nigeria, David Adeleke, maarufu kwa jina la Davido, ameshangazwa na mpenzi wake Chioma Rowland kuwa na uwezo mkubwa wa kuchora picha.

Davido alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ambayo imechorwa na mrembo na kisha kumpa kama zawadi.

“Mke wangu amechora picha hii na kunipa zawadi, asante sana mpenzi wangu, sikuwa nawaza kama angeweza kufanya kitu kikubwa kama hiki, naweza kusema ana kipaji cha hali ya juu, amenishangaza kwa kweli,” aliandika msanii huyo.

Miezi kadhaa iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba wawili hao wapo kwenye mipango ya kufunga ndoa mwaka huu, lakini kutokana na janga la corona mipango hiyo inashindwa kukaa sawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here