Chris Brown aonesha mapenzi kwa Ammika

0
568

NEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ameshindwa kuzuia hisia zake na kuamua kuanika mapenzi yake kwa mama wa mtoto wake Ammika Harris katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa.

Mwishoni mwa wiki iliopita mrembo huyo alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, hivyo Chris alianza kwa kuelezea jinsi wawili hao walivyokutana na kuanza uhusiano na kisha kupata mtoto ambaye anajulikana kwa jina la Aeko.

“Mara ya kwanza kukutana na wewe uliamua kuniambia hisia zako na kisha nikakuambia na mimi, niliamua kuachana na mambo mengine kwa ajili yako, mwambie mama yako nakupenda sana.

“Hii ni siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu, mtu mwingine wa pekee ambayo anakuangalia kama ninavyofanya mimi ni Aeko,” alisema msanii huyo.

Wawili hao walifanikiwa kumpata mtoto huyo Novemba 20 mwaka 2019, lakini wawili hao hawakai pamoja, Ammika anaishi nchini Ujerumani na Chris anaishi Los Angeles, Marekani, ila msanii huyo amedai umbali wao sio tatizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here