Snoop Dogg amjia juu 6ix9ine

0
636

CALIFORNIA, MAREKANI 

RAPA Snoop Dogg amemjia juu rapa chipukizi Tekashi 6ix9ine baada ya kijana huyo kuonekana akiangalia kipande cha video cha Suge Knight akimshambulia Snoop kwa kumwambia ni ‘snichi’

Video hiyo ilikuwa ya miaka ya nyuma ambapo ilileta utata kati ya rapa Snoop na Suge Knight, hivyo kitendo alichokifanya Tekashi 6ix9ine kimelata mjadala mkubwa.

Hata hivyo Tekashi 6ix9ine alikwenda mbali zaidi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwauliza mashabiki zake kama wapo tayari awatajie masnichi ambao walisababisha yeye kwenda jela.

“Sina tatizo na Suge Knight, kila kitu kilikwenda sawa, lakini kwa sasa naweza kusema kuna wasanii ambao wanataka kuzisukuma nyimbo zao ziweze kufanya vizuri kwa kuwachokoza wengine, sina muda huo, lakini mambo yakizidi nitajua nini cha kufanya,” aliandika Snoop.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here