25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Dar hatarini kupata magonjwa ya mlipuko

Nora Damian -Dar es salaam

JIJI la Dar es Salaam lipo hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko baada ya mtambo wa kusukuma taka katika dampo la Pugu Kinyamwezi kuharibika na kusababisha taka kurundikana mtaani.

Kutokana na hali hiyo, magari yamekuwa yakichukua wastani wa siku moja hadi tatu kumwaga taka, huku mengine yakishindwa kufanya safari zaidi ya moja.

Akizungumza jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri wa Manispaa ya Ilala, Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira, Sultan Salim, alisema zaidi ya tani 1,100 zinazalishwa kila siku katika manispaa hiyo na uwezo wa kuzoa ni kati ya asilimia 55 hadi 65.

“Jana (juzi) taka zilianza kumwagwa saa 3 usiku, leo (jana) haijulikani zitamwagwa saa ngapi, ukitokea mlipuko wa magonjwa sisi madiwani na mkurugenzi ndio tutakaowajibika, dharura inahitajika kwa haraka kunusuru usafi wa mazingira na kulinda afya ya jamii,” alisema Salim ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki (CCM).

Alishauri miundombinu ya dampo hilo iboreshwe na kuitaka manispaa itenge eneo lake.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Jumanne Shauri, alisema watatafuta eneo kwa ajili ya dampo la muda kuepuka kukumbwa na magonjwa ya mlipuko.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles