29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbatia aanza ziara kivingine, azuiwa kwa muda

Eliud Ngondo -Mbeya

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, ziara yake ya kichama mkoani Mbeya imekatishwa kwa muda na kuhojiwa na polisi kwa takribani dakika 33.

Hatua hiyo inakuja licha ya juzi Mbatia kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, na kufanya naye mazungumzo jambo ambalo kwa siku za karibuni halijazoeleka sana kwa viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakilalamikia wakuu wa mikoa na wilaya kuwazuia kufanya shughuli zao za kisiasa.

Mapema jana, Mbatia alisema amezuiwa kufanya mkutano wa ndani katika Kijiji cha Kandete, Kata ya Kandete wilayani Rungwe na kutakiwa kwenda Kituo cha Polisi Lwangwa kuripoti.

Hayo yametokea jana wakati Mbatia akiendelea na ziara yake katika Mkoa wa Mbeya ambayo amekuwa akifanya mikutano ya ndani na wanachama wa chama hicho.

Mbatia alisema juzi alifanya mkutano katika Jimbo la Rungwe ambako ndiyo makao makuu ya wilaya, lakini jana alipofika kufanya mkutano wa ndani, alipatiwa taarifa ya kutokuendelea na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi Lwangwa.

Alisema kutokana na wito huo, alienda kusikiliza kwani ni wajibu wa kuitikia wito wa aina yoyote ile na kusikiliza madhumuni makubwa ya wito huo.

“Mimi ninafanya mikutano ambayo imekubaliwa kisheria na Serikali, hivyo sioni kosa langu la kuitwa kwenda kuripoti katika kituo cha polisi wakati sijafanya mkutano wa ndani,” alisisitiza Mbatia.

Alisema licha ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kumtaarifu kufanya ziara ndani ya mkoa huo, lakini yeye hakuwa mtu wa kutoa kibali, hivyo jambo la kuitwa na polisi linatakiwa kutokupuuzwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles