27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

RC atembelea wanaotengeneza gongo na kuchukua sampuli

Florence Sanawa -Mtwara

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema pombe ya kienyeji aina ya gongo, inaweza kutumiwa kama rasilimali muhimu viwandani, baada ya wataalamu mbalimbali kusema inaweza kutumika kama spiriti ya kusafishia vidonda.

Kutokana na hilo, Byakanwa imemlazimu kuchukua sampuli mbalimbali kwa vipimo na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Alisema hatua hiyo ni kuelekea uchumi wa viwanda.

Byakanwa alisema mkoa wake umejipanga kukuza uchumi kwa kutumia zao la korosho na kuona namna bibo litakavyoweza kuboresha uchumi.

Akizungumza baada ya kutembelea watu mbalimbali wanaotengeneza pombe za kienyeji, ikiwemo gongo jana, alisema kinywaji hicho ambacho sio rasmi, kimekuwa kikitengenezwa kwa kutumia mabibo makavu.

Alisema kutokana na hili ilimlazimu kuwatembelea ili kuona namna pombe hiyo inavyotengenezwa na kuchukua sampuli na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Alisema mabibo makavu yamekuwa yakitumika kuzalishia juisi, mvinyo na jam, huku wengine wakitumia kuzalishia gongo ambayo hatua za awali imeonyesha inaweza kutumiwa kama spiriti na mbolea shambani.

“Unajua wapo watu wanaodhani nataka kuhalalisha pombe za kienyeji, wapo wanaokwepa wakidhani watakamatwa,  baada ya kutoka hapa, nawatoa hofu kuwa zao la korosho linaweza kutuongezea viwanda na ajira, ndiyo maana nafanya mchakato wa kushirikiana na ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuchukua sampuli mbalimbali za gongo na kuzipima ili kujua nini matumizi sahihi ya pombe hiyo.

“Mnaweza kuwa na rasilimali muhimu yenye thamani kwa matumizi ya binadamu na nyingine viwandani msijue, ndiyo maana tunaangalia namna ya kuongeza thamani, kupima na kujiridhisha ili kuona gongo inafaa kwa matumizi ya binadamu ama viwandani,” alihoji Byakanwa.

Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kusini, Eliamini Mkenga alikiri kupokea sampuli hizo na kusema uchunguzi utafanyika, kikubwa ni kuangalia iwapo itafaa kwa afya za watumiaji.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles