24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

CUF yadai kuvuna wanachama zaidi ya 1000 Pemba

Amina Omari – DAR ES SALAM

CHAMA  Cha Wananchi CUF kimesema kimepata heshima kubwa baada ya kufanikiwa kurejesha ngome yao kisiwani Pemba ambako kimepokea wanachama wapya 723 waliokabibidhiwa kadi za CUF.

Zaidi kimesema idadi hiyo inajumuisha wananchama 604 waliorudisha kadi za chama cha ACT-Wazalendo na kuamua kurejea CUF.

Kauli hiyo imetolewa na Mohammed Ngulangwa ambaye ni Mkurugenzi wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma wa  CUF wakati wakiongea na waandishi wa habari jijini Daresalaam.

Alisema ziara hiyo ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba imewajengea heshima kubwa kwa kukiwezesha chama hicho kurejesha ngome yake visiwani humo na kuongeza hamasa kwa wanachama.

Ngulangwa amesema kutokana na kufanikiwa kwa ziara hiyo ya Profesa Lipumba, nguvu ya Maalim Seif imeweza kumomonyoka kisiwani humo.

Amesema mkakati wa kukiangusha CUF ulioratibiwa na watu waliopora mali za chama hicho visiwani Zanzibar unaelekea kukwama.

”Lengo la mpango huu wa hujuma ni kukifaidisha chama kilichopora mali na ofisi za CUF hatuko tayari kuendelea kuvumilia mchezo huu wa kukihujumu chama hivyo tutaendelea kusimama imara kwa maslahi ya wananchi,”alibainisha Ngulangwa.

Aliongeza kuwa miongoni mwa wanachama waliorejea CUF walidhihirisha kujutia maamuzi yao waliyoyafanya bila kutafakari.

Alisema kutokana na mafanikio hayo aliyopata Profesa Lipumba kisiwani Pemba maadui wa chama hicho wamepatwa na mshtuko na mfadhaiko.

Alisema chama hicho kimefanikiwa kupata habari za uhakika kwamba viongozi wa kubwa wa chama kilichopora ofisi za CUF huko Pemba wamekuwa na mazungumzo ya kupanga hujuma dhidi ya chama.

Alisema mazungumzo hayo ambayo yanawahusisha baadhi ya wanachama na viongozi wa CUF waliorubuniwa mwanzoni yalilenga kuzuia kabisa ziara ya Profesa Lipumba, Pemba ili kudumisha ulaghai na hadaa kwamba CUF haipo kisiwani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles