27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Chris Brown awaliza mashabiki

ST. LOUIS, MAREKANI

MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, mwishoni mwa wiki iliopita aliwaliza mashabiki zake huku St. Louis, Missouri kutokana na jinsi alivyo wapagawisha kwenye shoo yake.

Msanii huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya albamu yake mpya ya Indigo kwenye miji mbalimbali nchini Marekani, hivyo baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye shoo hiyo katika ukumbi wa Enterprise Center, walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakitokwa na machozi kwa kuguswa na muziki wake.

Msanii huyo alitumia dakika 90 jukwaani kuwapa burudani mashabiki zake kwenye ukumbi huo ambao unachukua zaidi ya watazamaji 18,400. Chris aliimba nyimbo 14 kutoka kwenye albamu hiyo mpya yenye nyimbo 32.

Miongoni mwa nyimbo ambazo aliziimba ni pamoja na No Guidance, Heat, Back to Love, Urgundy, Don’t Check on Me, Liquor, Drunk Texting na Show Me.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles