Rostam wamtuliza Shilole

0
1138

JESSCA NANGAWE

BAADA ya msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kuwatolea maneno makali wasanii wanaounda kundi la Rostam, Roma Mkatoliki na Stamina, kutokana na kile walichokiimba kwenye wimbo wao wa Kijiwe Nongwa, wasanii hao wamesema hawana ugomvi na mrembo huyo wala shemeji yao Uchebe.

Akizungumza na MTANZANIA, Stamina alisema Shilole kwao atanedelea kuwa dada yao na wataendelea kutaniana naye kwa kuwa ni sehemu ya kazi yao.

“Shilole ni dada yetu na tunamtania sana, hata wakati tunatoa hii nyimbo tulijua atajibu ila hatuna tatizo nae kwani tuna heshimiana sana na tunataniana sana,” alisema Stamina.

Baada ya Rostam kumtaja Shilole kwenye wimbo huo, mrembo huyo aliwajia juu na kuamua kuandaa wimbo kwa nia ya kuwajibu kwa kile alichodai amevunjiwa heshima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here