33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kipa Tottenham kukaa nje hadi 2020

LONDON, ENGLAND

UONGOZI wa timu ya Tottenham umethibitisha utaikosa huduma ya mlinda mlango wake Hugo Lloris hadi 2020 baada ya kupata tatizo la kugeuka kiwiko kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brighton mwishoni mwa wiki iliopita.

Katika mchezo huo, Tottenham ambao walikuwa ugenini walikubali kichapo cha mabao 3-0, lakini mlinda mlango huyo hakuweza kuumaliza mchezo huo kutokana na kuumia na kisha kutolewa nje.

Kupitia website ya Tottenham, uongozi wa timu hiyo umedai mchezaji huyo amepata tatizo ambalo litaweza kumuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

“Hugo Lloris ataendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na tatizo alilolipata la kugeuka kiwiko kwenye mchezo wetu dhidi ya Brighton mwishoni mwa wiki iliopita.

“Kutokana na uchunguzi wa awali mchezaji huyo anaweza hasifanyiwe upasuaji wowote kutokana na hali hiyo, lakini nahodha huyo hawezi kurudi kufanya mazoezi na timu hiyo kabla ya kumalizika kwa mwaka 2019.

“Mchezaji huyo atakuwa nje huku akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa kipindi chote hadi pale atakapokuwa fiti kurudi viwanjani,” waliandika Tottenham.

Tottenham kwa sasa wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 11 baada ya kucheza michezo nane.

Hata hivyo, kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amedai kumkosa mlinda mlango huyo ambaye alibeba taji la Kombe la Dunia mwaka jana nchini Urusi ni pigo kubwa kwake hasa kwenye michezo ya kuwania kufuzu Euro 2020 dhidi ya Iceland na Uturuki, lakini ni nafasi kwa makipa wengine kuonesha uwezo wao.

“Hatokuwepo kwenye kikosi chetu, hivyo tutakuwa kwenye wakati mgumu wa kufuzu, yeye ni mchezaji muhimu sana kwetu, lakini ninaamini wachezaji waliopo wanaweza kuziba nafasi hiyo,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles