25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Chapakazi watoa zawadi ya mwaka mpya

Ramadhan Hassan,Dodoma

Kikundi cha kutunza na kuhifadhi mazingira cha (Chapakazi) cha jijini Dodoma kimetoa zawadi ya mwaka mpya wa 2021 kwa wateja wake ambayo ni punguzo la bei ya miche ya matunda na vivuli lengo likiwa ni kuendelea kulifanya Jiji la Dodoma kuwa la kijani.

Hayo yameelezwa leo Desemba 28, Jijini hapa na Mtunza Fedha wa Kikundi hicho, Darwesh Said alipozungumza na Waandishi wa Habari.

Darwesh amesema kutokana na dhamira ya Kikundi hicho kuwa ni kuhakikisha Dodoma inakuwa ya kijani imetoa punguzo la asilimia 20 ya miche yote inayouzwa katika eneo lao lililopo barabara ya Iringa.

Amesema miche ya miembe ambayo awali ilikuwa ikiuzwa kwa Sh 5,000 sasa itauzwa kwa Sh 4,000.

Darwesh amesema miche ya miparachichi, michungwa, ndimu na limao iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh 5,000 sasa itauzwa kwa Sh 3,000.

Kwenye miche ya vimvuli amesema itauzwa kwa Sh 2,000 ambapo awali ilikuwa ikiuzwa kwa Sh 3,000.

Hata hivyo, Darwesh amewaahidi wakazi wa Dodoma kuwa wataendelea kupata miche bora kutoka katika Kikundi hicho kwa mwaka ujao wa 2021.

“Kwanza tunawatakia Sikukuu njema, kikubwa tunawahamasisha kuendelea kupanda miti ili kutunza mazingira, ahadi yetu kwa wateja wetu ni tutaendelea kuhamasisha upandaji wa miti na sisi tunawaomba Watanzania wapande miti,”amesema Darwesh.

Katika hatua nyingine, Darwesh amesema wameendelea kutoa huduma za maharusi kupiga picha katika bustani yao iliyopo barabara ya Iringa ambapo amewashauri maharusi ambao wanatarajia kufunga ndoa kufika katika eneo hilo.

“Hapa kuna kila sehemu ya kupiga picha,bustani yetu ina ubora wa hali ya juu,watapigwa picha za kila aina hapa,”amesema.

Pia, amesema vinapatikana vyungu vya kisasa katika eneo hilo kwa ajili ya Kupamba nyumba na maeneo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles