Wazazi watakiwa kusimamia vyema elimu ya watoto

0
153

Na Shomari Binda, Musoma

Wazazi na walezi wametakiwa kusimamia vyema elimu ya watoto wanapokwenda kuanza kidato cha kwanza ili waweze kufikia ndoto zao.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkurugenzi wa kutuo cha Elimu na Mafunzo ya Ujasiriamali cha “Bismart Education Centar”, Boniphace Ndengo, wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wanaokwenda kujiunga na kidato cha kwanza.

Amesema kupitia kituo hicho wamewaandaa vyema wanafunzi wenye ndoto mbalimbali za kufika mbali hivyo ni vyema wazazi na walezi kuzisimamia.

Nao, baadhi ya wazazi na walezi waliozungumza na Mtanzania Digtal wamesema wamelidhushwa na mafunzo waliyopata watoto wao ambapo kwa muda mfupi wamekuwa na madiliko makubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here